Ngiri ni nini?
Ngiri ya kinena hufahamika kwa Kiingereza kama Inguinal Hernia. Ngiri katika eneo la kinena hutokea pale utumbo hujitokeza kwenye uwazi katika ukuta wa tumbo kwenye kinena. Ngiri kwenye kinena hutokea mara nyingi na huwaathiri zaidi wanaume.
Dalili kuu ni uvimbe kwenye kinena, ambao ukisukumizwa ndani unapotea kwa muda. Utambuzi hufanywa na daktari kwa kuchunguza uvimbe kwa kutumia kipimo cha ultrasound. Hali hii isipotibiwa inaweza kusababisha utumbo kunaswa na hivyo kushindwa kupatiwa damu na hatimaye kuoza. Hali hii hurekebishwa kwa upasuaji. Ngiri iliyonaswa ni hali ya dharura na inahitaji matibabu ya dharura kwa njia ya upasuaji.
Dalili za ngiri
Dalili za ugonjwa wa ngiri ni pamoja na uvimbe kwenye eneo la kinena au kifuko cha korodani. Uvimbe huu unaweza kusababisha maumivu, hasa wakati wa mazoezi. Uvimbe unaweza kupotea kwa muda mrefu pale unaposukumizwa ndani lakini baadaye hurejea.
hicho hakitakiwi kuwepo. Ngiri ya kinena hutokea pale utumbo mdogo unapopita katika uwazi katika ukuta wa tumbo na kutokelezea kwenye kinena.
Uwazi huu unaweza kutokea kabla ya kuzaliwa, au baada ya kuzaliwa kutokana na umri, jeraha au udhaifu wa misuli. Vitu vinavyoongeza shinikizo kwenye tumbo, kwa mfano unene wa kupita kiasi, kikohozi cha muda mrefu, kujikamua sana wakati wa haja kubwa au kubeba vitu vizito, huongeza uwezekano wa kupata hali hii.
Hali hii kwa kawaida hujitokeza zaidi kwa wanaume, na watu wenye umri wa makamo. Hii ina maana hata wanawake pia hupatwa na hali hii.
Matibabu
Inasemekana kua hakuna njia ya kutibu ugonjwa wa ngiri ispokua kwa uasuaji, lakini leo hii kampuni ya ETERNAL INTERNATIONAL Kutoka china , imefanikisha kutibu magonjwa mengi bila upasuaji ambayo yalipaswa kupasuliwa ikiwemo ngiri.
Kinga
Kuepuka shughuli ambazo huongeza shinikizo katika tumbo, kama vile kujikamua wakati wa haja kubwa au kubeba vitu vizito, huweza kuzuia kupata hali hii, au huweza kuzuia ngiri kuwa kubwa zaidi.
Ubashiri
Upasuaji kwa kawaida hutibu hali hii. Ngiri isipotibiwa, huweza kusababisha utumbo kunaswa, ambayo mara nyingi husababisha maumivu makali, utumbo kuvimba au sehemu za utumbo kuoza. Hii inaweza kuhatarisha maisha.
Jiunge whatsapp kupata elimu ya afya
https://chat.whatsapp.com/Kdbqqe1TWCn10djL2rnQBC
==============================
Kwa kupata huduma za matibabu au vipimo kujua afya yako wasiliana nasi
+255 626 908 654
+255 718 958 410
Majumbasita Dar es salam

Comments
Post a Comment