Skip to main content

Posts

Showing posts from 2024

SARATANI YA TEZIDUME

SARATANI YA TEZI DUME Tezi dume ni nini? Tezi dume ni tezi inayopatikana kwa jinsia ya kiume. Tezi hii ina kazi ya kutengezeza majimaji meupe mepesi yenye unato kidogo. Majimaji haya husaidia mbegu za kiume kutembea kwa urahisi. Ipo wapi? Tezi dume iko mwishoni mwa kibofu cha mkojo. Pia inauzunguks mrija unaounganisha kibofu cha mkojo na na mrija wa mkojo wa uume (urethra) na iko mbele kidogo ya utumbo mpana ndani ya fupa la nyonga. MIONZI. Sawa na upasuaji inaweza kuondoa ugonjwa iwapo haujasambaa. Mionzi pia hutolewa kama tiba shufaa. DAWA YA SARATANI Baadhi ya wagonjwa hufaidika na tiba hii, dawa hutolewa kwa muda mfupi na kufuatilia maendeleo ya mgomjwa kwa kufanya PSA,dawa inaweza kuwa moja au mchanganyiko. HOMONI Hutolewa mfullulizo kwa njia ya vidonge au sindano. Ufuatiliaji wa karibu Ni muhimu kufuatilia hali ya tezi isirejee baada ya ugonjwa kutibiwa kwa kufanya kipimo cha PSA mara kwa mara angalau miezi mitatu mara moja. Athari zitokanazo na matibabu mbalimb...

FAIDA ZA KUSHANGAZA ZA KULA PAPAI AMBAZO PENGINE HUKUZIJUA

FAIDA ZA KULA PAPAI KILA SIKU Chanzo bbc.com ongea na mtaalamu wako wa afya  Papai ni tunda la kushangaza na lenye afya. Ina 'antioxidants' ambayo hupunguza kuvimba na kupambana na magonjwa na kusaidia mtu kuonekana na umri mdogo. VIRUTUBISHO VYA PAPAI Kalori, Wanga, Nyuzinyuzi, Protini, Vitamini C, Vitamini A, Vitamini B9, Potasiamu, Kalsiamu na Magnesiamu. FAIDA ZA KIAFYA ZA PAPAI Huzuia Saratani :  Utafiti unaonyesha kuwa 'lycopene' iliyomo kwenye papai inaweza kupunguza hatari ya saratani. Inaweza pia kuwa muhimu kwa watu wanaopata matibabu ya saratani. Papai lina wingi wa vitu vya kuzuia saratani ikiwa ni pamoja na folate, vitamini C, beta-carotene na vitamini E ambayo hupunguza hatari ya saratani. Utafiti mdogo uliofanywa kwa watu wazima wenye kuvimba na shida ya tumbo, ulipunguza madhara ya msongo na seli za saratani. Hata hivyo, utafiti zaidi unahitajika kabla ya kufikia hitimisho. Cholesterol na Afya ya Moyo:  Tafiti zimeonyesha kuwa matunda na mbomboga zenye ...

KWANINI SIPATI UJAUZITO?

kwanini sipati ujauzito? ‘Kwa kawaida mwanamke anatakiwa apate ujauzito ndani ya mwaka mmoja baada tu ya kuolewa au kuanza mahusiano na yule ambaye tayari ana mtoto. Tunategemea baada ya miaka miwili hadi mitatu baada ya kupata mtoto apate mwingine labda kama hajaamua yeye pamoja na mumewe. Ujauzito unapatikana baada ya kufanya tendo la ndoa kwa ukamilifu, yaani katika kipindi ambacho mwanamke anaweza kupata ujauzito wengine wanaita siku za hatari lakini kitaalam tunaita siku za ‘Ovulations’. Suala hili pia linaangalia kwa upande wa pili wa mwanaume ambaye pia tunategemea ana uwezo huo wa kumpa mwanamke mimba kwa kuwa na mbegu zenye ubora na awe na nguvu za kutosha za kufanya tendo ili mwenzi wake apate ujauzito. Kitendo cha kukaa muda mrefu bila ya kupata mtoto huku mkiwa mnamtafuta huitwa ugumba kwa hiyo unahitaji uchunguzi na tiba. Picha inaonesha mtoto akiwa Karibu na kuzaliwa Wasiliana na dokta wako CHANZO CHA MATATIZO Mwanamke kutopata ujauzito husababishwa na matatizo mengi kwa ...

KUKOSA CHOO, AU KUPATA CHOO KWA TABU

NAAMINI WENGI WANATESEKA NA TATIZO HILI LA KUKOSA CHOO AU KUPATA KWA HALI YA TABU IKIAMBATANA NA MAUMIVU.  SULOMY HEALTHCARE IMEKUANDALIA DOZI NZURI YA KUTATUA SHIDA HIO NA KUKUFANYA UISHI NA AMANI KAMA WENGINE.  DOZI YETU NI YA WIKI TATU TU UNATUMIA,  BAADA YA HAPO UNAKUA UMEMALIZA TATIZO LAKO.  DOZI HII ITAGHARAMIWA KWA SHILINGI 30,000/=  MIONGONI MWA WATUMIAJI WA DOZI ZETU. Ushahidi ni muhimu kuwepo ili kumpa tumaini mteja wetu ahisi yupo mahali salama.  1: shuhuda WA kwanza:- Zilikosekana sms za awali kwa sababu ya kufutika kwa baadhi YA sms, Ila ni baadae YA kutumia dawa yetu nikamuuliza Hali yake na majibu yake yakawa kama hivyo.  2: shuhuda WA pili:- Alitumia dozi ya Kulainisha Choo, pamoja na Bawasiri, na huo mlolongo wa matumizi yalivyoenda,  na tunashukuru mungu amepona na kapata faida nyengine za tiba ambazo hakuzitarajia.  KWA kuepusha kurefusha post tutosheke na shuhuda hizo mbili.  USHAURI WA BURE PENDELEA SANA KUTUMIA MBOGAMBOGA NA MATUNDA KABLA YA KUANZA KULA KWA DAKIK...

JUA UGONJWA WA KISUKARI,CHAZO CHAKE,DALILI NA TIBA YAKE

JUA UGONJWA WA KISUKARI,CHAZO CHAKE,DALILI NA TIBA YAKE Magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni magonjwa ambayo hayasambazwi kwa mtu mwingine kwa kuwa hakuna vimelea mwilini vinavyohusiana na magonjwa hayo. Magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni kama ya moyo na mishipa ya damu, figo, saratani, kifua sugu, kisukari, magonjwa ya akili na mengine ya kurithi kama vile ugonjwa wa selimundu (Sickle Cell Disease). Ripoti ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) ya 2013, inadai magonjwa yasiyo ya kuambukiza ndio chanzo kikubwa cha vifo ulimwenguni, yakifanya asilimia 63 ya vifo vyote kwa mwaka. Magonjwa yasiyo ya kuambukiza huua watu zaidi ya milioni 36 kila mwaka. Asilimia 80 ya vifo vinasababishwa na magonjwa hayo hutokea nchi zinazoendelea, Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi hizo. Inakisiwa kuwa mwaka 2020 magonjwa haya yasiyo ya kuambukiza yatasababisha asilimia 73 ya vifo vyote duniani na asilimia 60 ya ukubwa wa tatizo la magonjwa duniani. Nchini Tanzania, katika mpango wa upimaji wa afya kwa magonjwa yasi...

TATIZO LA NGUVU ZA KIUME

MWANAMME BILA NGUVU ZA KIUME, NI MTIHANI MKUBWA Moja ya Matatizo yanayoharibu afya ya uzazi wa mwanamme ni ukosefu wa nguvu za kiume,  na kutokana na hilo hupelekea hata kuathirika kisaikolojia kwa mwanamme. -Mishipa ya damu. -Mfumo wa neva za fahamu. -Mfumo wa hormon na vichocheo vya mwili. Vitu hivyo ni miongoni mwa vitu vinavyoshirikiana kwa pamoja ili uume uweze kufanya kazi ipasavyo. Mazoezi ya mwili. Mlo wenye virutubisho kamili  Ni muhimu sana katika kujenga afya ya nguvu za kiume na afya kiujumla. SABABU ZA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME - Magonjwa ya moyo. -kuziba kwa mishipa ya damu. -Shinikizo la damu. -Ugonjwa wa kisukari. -Unene kupitiliza. -Matatizo ya ubongo. -Matumizi ya vileo. -Kutokupata muda wa kutosha kupumzika. -Magonjwa ya kiuno na uti wa mgongo. -Kujichua. -kutokufanya mazoezi. -Matumizi ya madawa ya kemikali kutibu nguvu za kiume. -Mawazo na wasiwasi. -Matatizo ya kibofu cha mkojo na tezidume. -Magonjwa ya kensa na vidonda vya tumbo. -Umri mkubwa. Nk. DALILI ZA UKOSE...

TATIZO LA KICHOMI NI MOJA YA DALILI ZA UGONJWA MOYO

TATIZO LA KICHOMI NI MOJA YA DALILI ZA UGONJWA MOYO VIJANA wengi leo wanapatwa na maradhi ambayo zamani yalikuwa ya wazee au watu wa makamo. Maradhi haya ni kama kisukari na mstuko wa moyo. Kichomi ni moja ya dalili za ugonjwa moyo. Kupatwa kichomi mara moja moja si vibaya. Ukipatwa muda mrefu au kila wakti ; basi chunguza zaidi. Bofya whatsapp Kichomi husababishwa au kinaweza kuwa . Dalili ya matatizo ya tumbo lenye asidi (acid) kuzidi Dalili za ugonjwa wa moyo uitwao Ischemic Jambo la kuangalia ni je? Unashikwa kichomi ukiwa unatembea? Umeinama au umelala Ukishakula chakula Kama unapatwa kichomi wakati ukitembea au ukishafanya mazoezi makali ina maana kuna tatizo la damu kuingia sawasawa au kuzunguka (circulation) katika moyo. Kama unapatwa kichomi baada ya kula ina maana kuna tatizo katika chakula unachokula. Je mlo wako una acid(uchachu) sana? Je, unakula vyakula vyenye pilipili na binzari(spices) kwa wingi sana? Kama una kula sana vyakula vyenye asidi ina maana tumbo lako halimen...

DALILI ZA TEZI DUME

Ni zipi dalili za ugonjwa wa tezi dume? Dalili za tezi dume zinaweza kuwa kali ama hafifu kutoka mtu hadi mtu. Ukali wa dalili hizi hautegemei ukubwa wa tezi. Inaweza kuwa tezi ni kubwa lakini dalili zisiwe kali. Miongoni mwa dalili za tezi dume ni:- 1.Kukojoa mara kwa mara, ama kuhisi kukojoa mara kwa mara 2.Kukojoa mara kwa mara wakati wa usiku 3.Kupatwa na uzgumu kutoa mkojo 4.Mchirizi wa mkojo kuwa dhaifu 5.Mkojo kukatakata unapofika karibu a mwisho 6.Kujichafua wakati wa kukojoa 7.Kushindwa kumaliza mkojo kabisa. 8.Damu kwenye mkojo 9.Kushindwa kukojoa kabisa. 10.Kupata mkojo mchache sana Kuwa na dalili tajwa hapo juu pekee hakuwezi kukupa uhakika kuwa una tatizo la tezi dume. Kwani dalili tajwa hapo juu zinaweza kuambatananna shida nyingine za kiafya kwa mfano:- 1.Maambukizi ya UTI 2.Kuvimba kwa tezi 3.Kupunguwa ukubwa wa mrija wa mkojo 4.Kuwepo na vijiwe kwenye kibofu 5.Kuwa na shida kwenye mfumo wa neva ambazo hudhibiti ufanyaji kazi wa kibofu 6.Kuwa na saratani

MUHANGA MKUU WA PID NI MWANAMKE

PID NI UGONJWA GANI.? Ugonjwa wa PID Hauwezi Mpata Mwanaume Bali Mwanaume Anaweza kumwambukiza Mwanamke Ugonjwa huu wa PID. Maambukizi ya via vya uzazi vya mwanamke au ugonjwa wa PID "Pelvic inflammatory disease" Ni maambukizi ya bacteria kwenye Shingo ya uzazi, Mirija ya fallopia, Ovari na Tumbo la uzazi (Uterusi). Sababu kuu ya ugonjwa huu wa (PID) ni maambukizi yanayo sambazwa kwa kujamiiana (STIs). Dalili za ugonjwa huu wa (PID) huweza kujumuisha, Maumivu ya nyonga, Maumivu ya tumbo chini ya kitovu, Maumivu wakati wa tendo la ndoa, Homa kali, Na uchafu mzito mweupe na wenye harufu mbaya kutoka ukeni. Utambuzi wa ugonjwa huu hufanywa kulingana na dalili na uchunguzi wa sehemu za siri, Katika uchunguzi wa kitaalamu sampuli za majimaji au usaha huchukuliwa ili kutambua bacteria aliye pelekea maambukizi hayo. Maambukizi ya via vya uzazi vya mwanamke (PID) hutibiwa kwa antibiotics, Kumbuka kwamba tiba ya ugonjwa huu hutofautiana kulingana ukali wa maambukizi, Hivyo basi...

MIGUU KUWAKA MOTO

Miguu kuwaka moto ni nini? Ni hali ya kuhisi miguu kuwa ya moto na inauma, hali hii huweza kuwa ya maumivu madogo au makali na wakati mwingine unaweza ukakosa usingizi kabisa wakati wa usiku kwa sababu ya maumivu. Baadhi ya visababishi vya miguu kuwaka moto huweza kuambatana na moja kuhisi miguu inachoma kama sindano au mwiba na mbili kupata ganzi au vyote viwili. Ingawa uchovu au maambukizi kwenye ngozi huweza kusababisha miguu kuwaka moto kwa mda mfupi na kubadilika mwonekano wake wa kawaida(rangi), kuumia kwa mishipa ya fahamu ya neva huwa ni sababu kuu ya kusababisha miguu kuwaka moto. Kuumia kwa neva huweza kusababishwa na mambo mbalimbali kama kisukari , ulevi wa pombe wa kupindukia, sumu aina Fulani, upungufu wa madini na vitamin (vitamin B) , au maambukizi ya virusi vya ukimwi. Vifuatavyo ni visababishi vya miguu kuwaka moto kwa undani zaidi; Visababishi vya miguu kuwaka moto ni Ulevi wa kupindukia(pombe)-( ugonjwa wa kutumia pombe) Maambukizi ya fangas kwenye miguu Ugonjwa ...