Skip to main content

KWANINI SIPATI UJAUZITO?


kwanini sipati ujauzito?

‘Kwa kawaida mwanamke anatakiwa apate ujauzito ndani ya mwaka mmoja baada tu ya kuolewa au kuanza mahusiano na yule ambaye tayari ana mtoto.

Tunategemea baada ya miaka miwili hadi mitatu baada ya kupata mtoto apate mwingine labda kama hajaamua yeye pamoja na mumewe. Ujauzito unapatikana baada ya kufanya tendo la ndoa kwa ukamilifu, yaani katika kipindi ambacho mwanamke anaweza kupata ujauzito wengine wanaita siku za hatari lakini kitaalam tunaita siku za ‘Ovulations’.

Suala hili pia linaangalia kwa upande wa pili wa mwanaume ambaye pia tunategemea ana uwezo huo wa kumpa mwanamke mimba kwa kuwa na mbegu zenye ubora na awe na nguvu za kutosha za kufanya tendo ili mwenzi wake apate ujauzito.

Kitendo cha kukaa muda mrefu bila ya kupata mtoto huku mkiwa mnamtafuta huitwa ugumba kwa hiyo unahitaji uchunguzi na tiba.


Picha inaonesha mtoto akiwa Karibu na kuzaliwa
Wasiliana na dokta wako

CHANZO CHA MATATIZO
Mwanamke kutopata ujauzito husababishwa na matatizo mengi kwa upande wake au mumewe.

Kwa upande wa mwanaume, vyanzo vinaweza kuwa kukosa nguvu kabisa au kupungukiwa nguvu za kiume tatizo liitwalo, ‘Erectile Dysfunction,’ tayari tumelizungumzia katika makala zilizopita.

Mwanaume anaweza kutoa manii mepesi sana kiasi kwamba baada tu ya kumaliza tendo mwanamke akisimama zinamwagika au zinatoka.

Dalili nyingine ni pale manii zinapopimwa hospitali na kuonekana zipo chache sana au hazina nguvu. Matatizo haya pia tayari tumeshayaeleza hapo nyuma.

Kwa upande wa mwanamke, vyanzo vinaweza kuwa matatizo katika mfumo wa homoni au vichocheo mbalimbali vya uzalishaji na upevushaji mayai na mzunguko. Mwanamke mwenye tatizo hili hupoteza siku zake za hedhi, mzunguko wa hedhi huvurugika na asijue ratiba yake ya mzunguko.

Pia hupoteza hamu na raha ya tendo, maumivu wakati wa tendo, hapati ute wa uzazi. Matatizo mengine ni kuziba kwa mirija ya uzazi, uwepo wa uvimbe katika mfuko wa uzazi, kupata damu ya hedhi kwa muda mfupi sana yaani moja au mbili au zaidi ya siku saba.

Pia kuumwa tumbo chini ya kitovu mara kwa mara, kutokwa sana na uchafu ukeni ambao wakati mwingine huambatana na harufu mbaya na muwasho pamoja na maumivu wakati wa haja ndogo.

Matatizo ya kutokwa na uchafu ukeni na muwasho havihusiani na ugonjwa wa yutiai ‘UTI’ kama wengi walivyozoea.

Matatizo mengine yanayomfanya mwanamke asipate ujauzito anapohitaji ni kutokufahamu siku za kupata mimba. Ili kufahamu siku za kupata mimba lazima ufahamu kwanza mzunguko wako uko vipi, mada hii tutakuja kuiongelea katika makala zijazo.

Vile vile mwanamke ajue siku zake za ‘Ovulation’ au siku za ute wa uzazi. Ute wa uzazi upo wa aina tatu, kuna mwepesi, mwepesi wa kuvutika na mzito.

jiunge na group

wasiliana na dokta wako 

Comments

Popular posts from this blog

ZAN SULOMY SEAMOSS - UNGA WA MWANI ZANZIBAR

10,000/= Nunua hii Unga wa Mwani Halisi Kutoka Zanzibar kwa Afya na Kinga ya Mwili 20,000/= Nunua hii Ongeza Nguvu, Kinga ya Mwili na Afya Bora kwa Zan Sulomy Sea Moss, una madini ya asili zaidi ya 92, unakosaje kuweka imara ulinzi wa mwili wako.  Mwani ni zao la baharini, huota kwenye myamba ya bahari, na juu ya bahari, mwani una madini zaidi ya 90 muhimu kwa afya ya mwanadamu. 25,000/= Nunua hii Unga wa mwani unapatikana kwetu kwa ujazo tofauti, unga huu unatoka zanzibar upande wa pemba. Agiza sasa Je, unahisi uchovu mara kwa mara? Kinga ya mwili iko chini? Unataka kirutubisho asilia salama cha kuongeza nguvu na afya? Suluhisho ni Zan Sulomy Sea Moss – Mwani halisi kutoka Zanzibar wenye madini zaidi ya 90 muhimu kwa mwili. Weka oda yako sasa FAIDA ZA KUTUMIA MWANI ✔ Huongeza kinga ya mwili ✔ Husaidia afya ya tezi (thyroid) ✔ Huboresha nguvu za mwili ✔ Hupunguza uchovu ✔ Huboresha mmeng’enyo wa chakula Hii ni Bidhaa asilia 100% Imetengenezwa kwa viwango vya afya Inatumiwa na wateja...

KARIBU MATIBABU YA BAWASIRI.

Soma hadi mwisho kama unahitaji kupona bawasiri. BAWASIRI INAKUSUMBUA? Je, unapata maumivu wakati wa kujisaidia, kutokwa na damu au uvimbe sehemu ya haja kubwa? Bawasiri ni tatizo linaloweza kuathiri maisha ya kila siku na kusababisha usumbufu mkubwa ikiwa halitapatiwa ufumbuzi mapema. DALILI ZA BAWASIRI  ✔ Maumivu wakati wa kujisaidia ✔ Kutokwa na damu wakati wa haja kubwa  ✔ Kuwashwa au kuungua sehemu ya haja kubwa  ✔ Uvimbe au vinyama vidogo sehemu ya haja kubwa  ✔ Kukaa kwa muda mrefu kuwa na maumivu MADHARA YA BAWASIRI   ❌ Maumivu makali ya mara kwa mara  ❌ Kupoteza damu na kuishiwa nguvu  ❌ Kushindwa kukaa kwa muda mrefu  ❌ Kupungua kwa ufanisi kazini na kwenye shughuli za kila siku  ❌ Kuathiri hali ya kujiamini na maisha kwa ujumla Usipuuzie dalili! Bawasiri unaweza kuanza taratibu lakini ukasababisha maumivu makali, kutokwa na damu wakati wa haja kubwa, kuwasha na uvimbe sehemu ya haja kubwa. ❗ Baadhi ya sababu za bawasiri ni:  ✔️ Kufunga choo kwa muda mrefu (constipation) ...

SULOMY PELVICLINE POWDER (DAWA YA PID)

SULOMY PELVICLINE POWDER Ondoa Maumivu ya Tumbo Chini na Tatizo la PID kwa Njia ya Asili WENGI WAPO HATARINI KUPATA UGUMBA PASI NA KUJIJUA PID: ni ugonjwa hatari uliosababishwa na mashambulizi ya bakteria kwenye njia za uzazi za mwanamke.  Ugonjwa huu una madhara makubwa iwapo kama haujatibiwa mapema.  Je, unasumbuliwa na: - Maumivu ya tumbo chini mara kwa mara? - Uchafu usio wa kawaida ukeni? - Hedhi kuvurugika? - Harufu mbaya au maumivu wakati wa tendo? - Kuambiwa una PID lakini tatizo haliponi kabisa? Usijali tena… Sulomy PelviCline Powder imeandaliwa kwa mchanganyiko wa mimea tiba maalum kusaidia kusafisha na kuimarisha mfumo wa uzazi wa mwanamke. 40,000/= Sulomy PelviCline Powder ni nini? Ni unga wa asili (100% Herbal) uliotengenezwa kusaidia: ✔ Kupunguza maumivu ya tumbo chini ✔ Kupunguza uchafu ukeni ✔ Kusaidia kurekebisha mzunguko wa hedhi ✔ Kuimarisha afya ya kizazi ✔ Kuongeza kinga ya mwili Kwa Nini Uchague Sulomy? ✅ Imetengenezwa kwa mimea asilia na salama ✅ Haina kemikali ...