Skip to main content

Posts

TATIZO LA KICHOMI NI MOJA YA DALILI ZA UGONJWA MOYO

TATIZO LA KICHOMI NI MOJA YA DALILI ZA UGONJWA MOYO VIJANA wengi leo wanapatwa na maradhi ambayo zamani yalikuwa ya wazee au watu wa makamo. Maradhi haya ni kama kisukari na mstuko wa moyo. Kichomi ni moja ya dalili za ugonjwa moyo. Kupatwa kichomi mara moja moja si vibaya. Ukipatwa muda mrefu au kila wakti ; basi chunguza zaidi. Bofya whatsapp Kichomi husababishwa au kinaweza kuwa . Dalili ya matatizo ya tumbo lenye asidi (acid) kuzidi Dalili za ugonjwa wa moyo uitwao Ischemic Jambo la kuangalia ni je? Unashikwa kichomi ukiwa unatembea? Umeinama au umelala Ukishakula chakula Kama unapatwa kichomi wakati ukitembea au ukishafanya mazoezi makali ina maana kuna tatizo la damu kuingia sawasawa au kuzunguka (circulation) katika moyo. Kama unapatwa kichomi baada ya kula ina maana kuna tatizo katika chakula unachokula. Je mlo wako una acid(uchachu) sana? Je, unakula vyakula vyenye pilipili na binzari(spices) kwa wingi sana? Kama una kula sana vyakula vyenye asidi ina maana tumbo lako halimen...

DALILI ZA TEZI DUME

Ni zipi dalili za ugonjwa wa tezi dume? Dalili za tezi dume zinaweza kuwa kali ama hafifu kutoka mtu hadi mtu. Ukali wa dalili hizi hautegemei ukubwa wa tezi. Inaweza kuwa tezi ni kubwa lakini dalili zisiwe kali. Miongoni mwa dalili za tezi dume ni:- 1.Kukojoa mara kwa mara, ama kuhisi kukojoa mara kwa mara 2.Kukojoa mara kwa mara wakati wa usiku 3.Kupatwa na uzgumu kutoa mkojo 4.Mchirizi wa mkojo kuwa dhaifu 5.Mkojo kukatakata unapofika karibu a mwisho 6.Kujichafua wakati wa kukojoa 7.Kushindwa kumaliza mkojo kabisa. 8.Damu kwenye mkojo 9.Kushindwa kukojoa kabisa. 10.Kupata mkojo mchache sana Kuwa na dalili tajwa hapo juu pekee hakuwezi kukupa uhakika kuwa una tatizo la tezi dume. Kwani dalili tajwa hapo juu zinaweza kuambatananna shida nyingine za kiafya kwa mfano:- 1.Maambukizi ya UTI 2.Kuvimba kwa tezi 3.Kupunguwa ukubwa wa mrija wa mkojo 4.Kuwepo na vijiwe kwenye kibofu 5.Kuwa na shida kwenye mfumo wa neva ambazo hudhibiti ufanyaji kazi wa kibofu 6.Kuwa na saratani

MUHANGA MKUU WA PID NI MWANAMKE

PID NI UGONJWA GANI.? Ugonjwa wa PID Hauwezi Mpata Mwanaume Bali Mwanaume Anaweza kumwambukiza Mwanamke Ugonjwa huu wa PID. Maambukizi ya via vya uzazi vya mwanamke au ugonjwa wa PID "Pelvic inflammatory disease" Ni maambukizi ya bacteria kwenye Shingo ya uzazi, Mirija ya fallopia, Ovari na Tumbo la uzazi (Uterusi). Sababu kuu ya ugonjwa huu wa (PID) ni maambukizi yanayo sambazwa kwa kujamiiana (STIs). Dalili za ugonjwa huu wa (PID) huweza kujumuisha, Maumivu ya nyonga, Maumivu ya tumbo chini ya kitovu, Maumivu wakati wa tendo la ndoa, Homa kali, Na uchafu mzito mweupe na wenye harufu mbaya kutoka ukeni. Utambuzi wa ugonjwa huu hufanywa kulingana na dalili na uchunguzi wa sehemu za siri, Katika uchunguzi wa kitaalamu sampuli za majimaji au usaha huchukuliwa ili kutambua bacteria aliye pelekea maambukizi hayo. Maambukizi ya via vya uzazi vya mwanamke (PID) hutibiwa kwa antibiotics, Kumbuka kwamba tiba ya ugonjwa huu hutofautiana kulingana ukali wa maambukizi, Hivyo basi...

MIGUU KUWAKA MOTO

Miguu kuwaka moto ni nini? Ni hali ya kuhisi miguu kuwa ya moto na inauma, hali hii huweza kuwa ya maumivu madogo au makali na wakati mwingine unaweza ukakosa usingizi kabisa wakati wa usiku kwa sababu ya maumivu. Baadhi ya visababishi vya miguu kuwaka moto huweza kuambatana na moja kuhisi miguu inachoma kama sindano au mwiba na mbili kupata ganzi au vyote viwili. Ingawa uchovu au maambukizi kwenye ngozi huweza kusababisha miguu kuwaka moto kwa mda mfupi na kubadilika mwonekano wake wa kawaida(rangi), kuumia kwa mishipa ya fahamu ya neva huwa ni sababu kuu ya kusababisha miguu kuwaka moto. Kuumia kwa neva huweza kusababishwa na mambo mbalimbali kama kisukari , ulevi wa pombe wa kupindukia, sumu aina Fulani, upungufu wa madini na vitamin (vitamin B) , au maambukizi ya virusi vya ukimwi. Vifuatavyo ni visababishi vya miguu kuwaka moto kwa undani zaidi; Visababishi vya miguu kuwaka moto ni Ulevi wa kupindukia(pombe)-( ugonjwa wa kutumia pombe) Maambukizi ya fangas kwenye miguu Ugonjwa ...